Tuzungumze SIASA, MUHASSO

21Feb
kelvin George Feb. 21, 2024, 10:59 a.m.

Tuzungumze SIASA, MUHASSO

Siasa ya vyuoni ni siasa ambayo kwa namna moja ama nyingine huwa na tahashishi fulani, na hushabiana kwa mbalii na siasa ya nchi, hapa ndipo huzaliwa viongozi wa baadae kwa taifa letu. Leo ningependa kuongelea zaidi kuhusu siasa za MUHASSO,kwa sasa naona joto si joto na baridi si baridi , mambo yameanza kutaladari japo sio kivilee. Kwanza tujikumbushe kuhusu siasa za mwaka 2021/2022, mwaka huu nilibahatika kukaa na wanaharakati wa kisiasa kipindi hicho na nilianza kujifunza kutoka kwao mpaka pale nilipoona siasa sio kitu yangu kabisa.

Siasa za mwaka huo zilikuwa pambe na zilikuwa na ushindani wa wazi kabisa, kila mwanasiasa alijaribu kuvutia upande wake. Kiukweli ilifika wakati sikuwa na upande kabisa na kila mwanasiasa aliyekuja nilikubali kumsapoti. WanaMUHASSO wengi walihitaji kupata kiongozi atakaye watetea nakutatua changamoto zao kadhaa, baada ya uchaguzi ikapatikana serikali sitaki kuzungumzia sana ni nini kilitokea, ila ninaamini WanaMUHASSO wanamajibu.
Mwaka 2022/2023 siasa ya mwaka huu ilikua siasa poa sana, nikuibie tu siri nilipiga kura. Mwanzoni tulitegemea kuona ushindani mkubwa baina ya pande mbili, yaani upande wa bwana Machange(mtia nia nafasi ya Urais) na mwanamama Vanessa (mtia nia nafasi ya Urais) badala yake, upande mmoja uliishia kujitoa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Urais hivyo kufanya uchaguzi kuwa mwepesi na serikali ya MUHASSO ikajipatia rais wakike wa kwanza ambaye ni Vanessa Rutabana akiwa na makamu wake bwana Frank Foundation.
Niwe muwazi, hakika serikali hii nimeiona ikifanya jitihada nyingi katika kuleta mabadiliko ya kweli kwa wanaMUHASSO. Sitaki kusema kama shabiki  kwa maana hata mimi ilinigusa kwa namna moja amanyingine. Niseme tu bila kumung’unya maneno hakuna serikali ambayo itakuja na kufanya kwa usahihi asilimia mia, amini usiamini lazima tu kunasehemu tu itakwama, sasa kama serikali imejitahidi kufanya vizuri kwa nini isipongezwe! Mimi naipongeza serikali hii ya mwanamama Vanessa Rutabana kwa kutatua changamoto za wanafunzi na kujali maslahi yao.
Sasa tuzungumzie hizi harakati za chini chini za kuwania urais serikali ya MUHASSO. Tunatarajia uchaguzi mwezi wa tano kuelekea wa sita, bila kujali ni nani na nani? watagombania nafasi hio wanaMUHASSO tunatakiwakuzingatia haya yafuatayo kwaajili ya kumpata kiongozi sahihi:

01.Haiba ya Nidhamu
Kiongozi yoyote asiye na nidhamu huishia  kujiona  na pia kudharau wengine

02.Uadilifu na Uchapakazi
Kiongozi lazima awe muadilifu asijihusishe na ubadhilifu wa aina yoyote ile pia awe mchapakazi na kuhakikisha anatatua changamoto mbalimbali za wanafunzi wenzake.

03.Awe na Uwezo Wakujenga Hoja
Hii ni sifa muhimu sana kwa kiongozi yoyote mzuri.

04.Asiye na Skendo Ovu
Hapa tunasema chui kaficha makucha, akisha patauongozi utaipenda show

05.Msikivu
Hii ni sifa kubwa mno kiongozi lazima awe msikivu, asikilize maoni yawengine katika utendaji.

06.Awe na Hofu ya Mungu
Unaweza sema hii ndio point kuu, zingatia sana hii.

Vipo vitu vingi sana vyakuzingatia kwenye suala zima la kumpata kiongozi mzuri ambaye, atakupigania utakapopata changamoto. Kabla ya kumchagua jiulize JE atapokea simu yako ukiwa na changamoto? JE atakupambania iliusidisco? JE atatekeleza yote aliyoahidi? JE anamaanisha anachokiongea? JE hana maslahi binafsi? Ukishapata majibu sahihi sasa ruksa kuchagua upande wako.
Komenti chini hapo ni nani unamtizamia kuwa rais wa MUHASSO?

Comments (0)

  • No Comments


Write a Comment

For inquiries, partnerships, or contributions, please reach out to us today

+255 678 435 684 Contact Us
WhatsApp